Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Hassan Kimanta amemwagiza kamishina msaidizi wa magereza mkoa wa Arusha Willison Mandarasa kuhakikisha wanaongeza kiwango cha uzalisha wa chakula kwa ajili ya matumizi ya magereza.
Ameyasema haya alipokuwa akizindua rasmi mitambo ya mashine ya kuvunia mazao mbalimbali yakiwemo mahindi katika ofisi za magereza jijini Arusha.
Mashine hizo zitasaidia kuongeza kasi ya uvunaji na kupunguza muda wa uvunaji.
Aidha, ameshauri kuwa wakitumia vizuri mashine hizo wanauwezo wa kuvuna magunia 20 hadi 25 kwa heka badala ya maguni 18 ya awali.
Kutokana na matumizi hayo ya mashine amesema, sasa magereza wanauwezo wa kujitegemea katika chakula kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwanzo.
Akitoa taarifa fupi ya mashine hizo kamishina msaidizi wa magereza mkoa wa Arusha Willison Mandarasa, amesema jumla ya mashine hizo ni 3 zilizogharimu kiasi cha fedha million 347 ambazo zitapelekwa pia kwenye maeneo mengine.
Amesema mpaka sasa magereza mkoa wa Arusha una ekari 350 kwa ajili ya kilimo cha Mahindi,ekari 301 za Maharagwe na ekari 10 za kilimo cha mbogamboga.
Nae, kamishina msaidizi magereza Andrew Ntamamilo,amemshukuru kamishina wa magereza Suelemani Mzee kwa kuweza kutimiza azma ya Rais John Pombe Magufuli ya kuhakikisha magereza inajitegemea kwa chakula.
Amesema kwa mashine hizo kuletwa zitasaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa watu katika kipindi cha mavuno kwani watakaoitajika kwa sasa ni wachache sana na mashine hizo zitafanya kazi kwa kiwango kikubwa.
Magereza imetekeleza azma ya kujitegemea katika chakula kama maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli ya kuhakikisha magereza nchi nzima inajitegeme katika chakula.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa