Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumanne Novemba 26, 2024 ameongoza wananchi wa Arusha kwenye zoezi la Ufanyaji wa usafi kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha, akihimiza wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara kwenye maeneo yao ya kazi na kwenye makazi yao ili kufanya mandhari ya Mkoa wa Arusha kuvutia zaidi wageni na watalii.
Kwenye Soko la Kilombero, Mhe. Makonda amewakumbusha wananchi wa Mkoa wa Arusha pia kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji kura za kuchagua Viongozi wa serikali za mitaa hapo Kesho Novemba 27, 2024, ambapo tayari Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa siku ya mapumziko ili kuwaruhusu wananchi kushiriki kikamilifu katika upigaji kura.
Mhe. Makonda pia amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa na Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maximillian Irangyi kuanza mara moja kutatua changamoto za kutuama kwa maji ndani ya soko la Kilombero wakati wa msimu wa mvua pamoja na kuvuja kwa paa la soko hilo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa