• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA: MSIWACHAGUE VIONGOZI WATAKAOTOA RUSHWA..

Posted on: October 26th, 2024

Na Elinipa Lupembe

Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024, Mkuu wa mka wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewaasa wananchi wa mkoa huo, kuwakataa viongozi wanato rushwa ili wachaguliwe na kuwasisitiza wasifanye kosa hilo, kwa kuwa rushwa ni adui wa haki, lakini rushwa ni kinyume na mapenzi ya Mungu.

Mhe. Makonda ametoa rai hiyo, kwenye kijiji cha Tukusi kata ya Loksale wilaya ya Monduli wakati akizindua Mradi wa uchimbaji visima 30 vya maji mkoa huo na kuwasisitiza wananchi waliojiandikisha kujitokeza kupiga kura ya kuwachagua wenyeviti watakao waongoza kwa miaka mitano ijayo.

"Ukimchagua kiongozi aliyekupa rushwa, hutathubutu kumuhoji kwa jambo lolote kwa kuwa tayari ameshakulipa, umeuza uhuru wako wa miaka mitano kwa shilingi elfu 10 na hata maendeleo yakikosekana utalazimika kukaa kimya". Amesema.

Amewahimiza kuwakataa viongozi wanaotaka kuwa madarakani kupitia fedha na vizawadi ambavyo, havina thamani ya kura wanayoitoa, badala yake kuwachagua viongozi waadilifu, wazalendo na wenye uchungu na wenye mipangp ya maendeleo ya kijiji na vitongoji vyao.

Amewasisitiza kutambua kuwa kupitia Uchaguzi, Serikali imewapa nafasi ya kuwaweka viongozi wanaokwenda kuunda Serikali, hivyo Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anataka mwananchi wamsaidie kupata viongozi waadilifu ili waweze kushiriki katika kusimamia vema fedha za maendeleo, wawe sehemu ya kushiriki usimamizi wa  miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

"Migogoro ya mingi ndani ya vijiji, mitaa na vitongoji ikiwemo migogoro sugu ya ardhi na haiwezi kuisha kama tukiwachagua viongozi ambao wametoa rushwa, kiongozi anayetoa rushwa, anataka kurudisha pesa aliyokupa, msikubali kuhongwa na mgombea yoyote, utashindwa kumhoji, utakaa kimya mnapodhulimiwa, mnapokosa barabara, jitafakarini kwa nini tunafedhehesha heshima tuliyopewa na Serikali yetu kwa shilingi elfu 10". Amesema Mhe. Makonda

Hata hivyo, amewaasa  wagombea wa vyama vyote, wasikubali kutoa rushwa ili wachaguliwe, kwa kufanya hivyo, watajitenga na Mungu, baraka za Mungu zitaondoka na kuwataka kutambua dhamana kubwa wanayopewa na wananchi inahitaji uadilifu wa hali ya juu.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa