Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella amefungua Semina ya Waandishi wa Habari wa mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro ya uwasilishaji na uhamasishaji wa matumizi sahihi ya matokeo ya Sensa ya Watu Makazi kisekta iliyofanyika mwaka 2022
Mkuu huyo wa mkoa amefungua semina hiyo ya siku mbili inayofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Kalolini mkoani Arusha leo 24.10.2023 na kuwapongeza waandishi wa habari kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuelimisha na kuhamasisha wananchi kushiriki wkenye Sensa ya watu na Makazi 2022.
Amesema kuwa,Waandishi wa Habari ni sehemu ya Mafanikio ya Sensa ya Watu na Makazi 2022, elimu na hamasa waliyoitoa iliwafanya wananchi kuhamasika kushiri Sensa hiyo na kufanikiwa kwa zaidi ya asilimia 99
Hata hivyo amewataka waandishi hao kuendelea kushiriki awamu ya tatu ya Sensa hiyo ambayo inahusisha matumizi ya Takwimu sahihi za Sensa ya Watu na Makazi inayojumuisha idadi ya watu, idadi ya makazi na hali za Watu na Makazi, miundombinu, huduma za Jamii na maeneo yake, taarifa za kiuchumi na Kijamii
"Kama waandishi wa habari watatoa takwimu sahihi kwa kadri mtakavyojengewa uwezo na NBS, itaondoa changamoto za taarifa za upotoshaji ambazo zinatokana na watu kutokuwa na taarifa sahihi zinazosababisha migogoro isiyokuwa ya lazima kwenye jamii na Serikali" Amesema Mhe. Mongella.
PICHA ZA MKUTANO
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa