Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amemtembelea mwanamke wa kwanza kujifungua katika kituo cha Afya Sale wilaya ya Ngongoro Bi. Hosiana, mara baada ya jengo la kinamama na watoto kukamilika.
Awali serikali ilitoa fedha kwa ajili ya utanuzi wa zahanati ya Sale na kuwa kituo cha Afya ili kuongeza upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa ikiwemo huduma za kulazwa, upasuaji na uzazi.
Bi. Hosiana mama wa watoto watatu amesema kuwa watoto wawili alilazimika kufunga safari mpaka Waso umbali wa zaidi ya Km 50 kutoka eneo hilo ili kwenda kujifungua jambo ambalo liliwapa gharama kubwa za muda na fedha lakini wapo kinamama waliopoteza maisha kwa kuchelewa kupata huduma za kujifungua.
Hata hivyo amemshukuru Mama Samia kwa kuwajengea kituo cha afya, kituo ambacho kimewapunguzia mwendo na gharama za kufauata huduma mbali, lakini zaidi kimeondoa vifo vusisvyo vya lazima kwa wanawake na watoto wakati wa kujifungua.
"Sisi wanawake wa Sale tunamshukuru Rais wetu, mama Samia ametujali wakinamama, tuna uhakika wa afya za familia zetu, watoto wawili nilijifungulia Wasao, ukiwa huna pesa unaweza kupoteza maisha" Amesema Hosiana
#tutakufikiapopoteulipo
#ArushaFursaLukuki
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa