Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella ameridhishwa na maendeleo upya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi za halmashauri ya Ngorongoro mradi unaotekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 2.6.
Mhe. Mongella amempongeza uongozi wa halmasahuri ya Ngorongoro kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo ujenzi ambao hapo awali ulienda kwa kusuasua sana.
Amewataka amewapa watalamu wa halmasahuri hiyo siri ya mafanikio katika utenzaji kazi ni pamoja na kuzingatia nidhamu, usimamizi na ufuatiliaji wa mara kwa, mambo haya yanawezesha kufikia malengo ya shughuli zote za serikali.
"Siri kubwa ya mafanikio katika kazi yoyote, ni kuweka malengo na kuwa na nidhamu, usimamizi na ufuatiliji unakuwezesha kufanya tahmini ya kutambua hatua za ulikotoka, ulioo na unapoelekea" Amesisitiza Mhe. Mongella
Akisoma taarifa ya mradi huo, Msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Masasila Chigulu, ameeleza kuwa, jengo ghorofa moja, ujenzi wa jengo hilo umetekelezwa kupitia 'Force Account' chini ya Mkandarasi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), huku mradi huo ukitekelezwa kwa awamu tatu, na tayari umefikia asilimia 80 ya utekelezaji wake.
Ikumbukwe kuwa serikali imeendelea kuboresha mazingira ya bora kwa watumishi kwa kuzingatia masuala ya Utawala Bora na Rasilimali Watu.
.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa