Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella amewatembelea wagonjwa waliojifungua na kulazwa kwenye wodi ya kujifungulia, kwenye Kituo cha Afya Karatu, wilaya ya Karatu, leo 29 Desemba, 2023.
Mhe. Mongella licha ya kuwafariji wagonjwa hao, amewa zawadi ikiwa ni ishara ya upendo na kuwapongeza kina mama hao, kwa kujifungulia kwenye kituo cha kutolea huduma ya Afya, yakiwa ndio malengo ya Serikali ya kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi wakati wa kujifungua.
"Lengo la Serikali ni kupambana na changamoto ya wajawazito kujifungulia nyumbani, na kujifungulia kwenye vituo vya afya ambavyo vimejengwa na Serikali, licha ya kutoa matibabu kwa wagonjwa, lakini pia inakwenda kuondoa vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua".Amefafanua Mhe. Mongella.
Aidha, amewasisitiza wananchi wote kujivunia miundombinu ya afya iliyojengwa na Serikali kwa kuhakikisha wanatumia zahanati, vituo vya afya na hospitali zilizojengwa na Serikali kwa kuwa lengo la ke ni kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma za afya kwa kusogeza huduma hizo karibu nawananchi.
Awali, Mhe. Mongella yupo wilayani Karatu kwa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo kiskta katika wilaya hiyo.
#arushafursalukuki
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa