• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI KUTOA SHILINGI MILIONI 1 KWA WALIOPOTEZA MAISHA KWA AJALI ARUSHA

Posted on: February 25th, 2024


Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe.John V.K Mongela ametoa salamu za pole kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na Watanzania wote, kwa niaba ya Serikali kufuatia vifo vya watu 25, vilivyotokana na ajali ya gari iliyotokea jana jioni Februari 24, 2024 eneo la Ngaramtoni wilaya ya Arumeru.


Mhe. Mongella ametoa pole wa ndugu jamaa na marafiki waliokusanyika nje ya jengo la kuhifadhia maiti, kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, wakisubiri maelekezo ya Serikali kuhusu msiba huo mapema leo Februari 25, 2024.


Amesema kuwa, Serikali inatoa  shilingi milioni moja kwa kila marehemu, ikiwa ni ubani kwa ajili ya kugharamia shughuli za mazishi pamoja na kutoa jeneza kwa familia zitakazohitaji kulingana na imani za dini zao.


Amewasilisha salamu za pole kutoka kwa viongozi wakuu wa nchi, wakiongozwa na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye yupo safarini Namibia kushiriki mazishi ya kiongozi wa nchi hiyo. 


"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kwa wafiwa wote, na ameagiza tushirikiane kwa pamoja kama wanaArusha na kama watanzania, kuwafariji wenzetu, na kwamba Serikali iko pamoja na wafiwa wote, na ameagiza Serikali kutoa ubani wa shilingi milioni moja kwa kila marehemu kwa ajili ya kusaidia shughuli za mazishi pamoja na kugharamia matibabu ya majeruhi wote" Amesema Mhe.Mongella.


Aidha, Mhe. Mongella ameweka wazi kuwa, msiba huo ni wa watanzania wote na Serikali imetoa kibali kwa ndugu na familia za merehemu kuanza kuchukua miili kwa ajili ya mazishi na tayari baadhi yao wameanza kuchukua miili hiyo.


Hata hivyo Mhe. Mongella amebainisha kuwa Serikali imeandaa utaratibu wa kugharamia matibabu ya majeruhi 21 waliotokana na ajali hiyo, na wanaoendelea na matibabu tangu jana, madaktari na wahudumu wa afya wanapambana kuhakikisha wanarejea afya zao.


Kufuatia ajali hiyo jumla ya majeruhi 21 wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali mbalimbali huku majeruhi 11 wakiwa wamelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Arusha Mount Meru.


Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamshna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11 jioni, ambapo Lori lenye namba za usajili  KAS 943, likiwa na Tela lenye namba TF67, likitokea Namanga, lilipoteza mwelekeo na kugonga magari matatu.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa