• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAKOGA NYOYO ZA WALIMU ARUSHA....

Posted on: November 19th, 2023

Na Elinipa Lupembe.

Kufuatia mkakati wa Serikali ya awamu ya sita ya kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu, kupitia program ya kuboresha miundombinu ya shule za Sekondari nchini (SEQUIP), mpango unaoenda sambamba na ujenzi wa nyumba za walimu, umewagusa na kukoga nyoyo za walimu kwa kuona Serikali inawajali.

Wakizungumza na mwandishi wetu, Walimu wa shule ya Sekondari Kiutu, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha, wamethibitisha kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imekoga nyoyo za walimu nchini, kwa kuweka mazingira wezeshi  wanayowapa unafuu katika tendo na kufundisha na kujifunza shuleni.


Wamesema kuwa tofauti na hapo awali, Serikali iliwekeza zaidi, katika kuimarisha miundombinu ya wanafunzi na kuwaachwa walimu, jambo ambalo liliwapa wakati mgumu katika ufundishaji lakini Serikali ya Awamu ya Sita imeenda mbali zaidi kwa kuwajali wanafunzi na walimu pia.


"Tendo la kujifunza na kufundisha linakwenda pamoja unapomuacha mmoja kati yao nyuma, inakuwa ni ngumu kufikia malengo ya uhamishaji wa maarifa kati ya mwalimu na mwanafunzi, unatengeneza uwazi 'gape',tunachelea kusema Serikali imetutendea haki walimu" Wamesema walimu hao


Mw. Fedrick Komba, amesema kuwa, shule ya sekondari Kiutu, ni shule mpya imejengwa majengo yote ya shule pamoja na nyumba ya walimu yenye sehemu za kuishi familia mbili, jambo ambalo wanaamini litaongeza tija katika ufundishaji na kupandisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi..


Naye mwalimu wa Taaluma sekondari Kiutu, Mwl. Stanley Antony Mwampimbe,  amesema kuwa kuwepo kwa nyumba nzuri za walimu zinawapunguzia makali ya maisha kwa kulipa kodi pale wanapoishi nyuma za kupanga, wanatumia gharama kubwa kulipa kodi za nyumba..


"Hapa Arusha gharama za maisha ziko juu na kusababisha kodi za nyumba kuwa juu pia, uwepo wa nyumba za walimu zinatupunguzia makali ya maisha, kwa serikali kutupunguzia mzigo wa kulipa kodi, walimu wa sasa tunaweza kuwa na maisha mazuri kama watumishi wengine wa Umma" Ameweka wazi Mwl. Mwampimbe.


Awali serikali kupitia mpango wa SEQUIP imejengea nyumba ya walimu yenye sehemu ya kuishi familia mbili (2in1), kwa shilingi milioni 98, shule ya sekondari Kiutu, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020 -2025.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa