• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI YAHIMIZA MATUMIZI YA MFUMO WA MANUNUZI YA UMMA - NeST

Posted on: September 9th, 2024


Na Elinipa Lupembe 



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko, amewaagiza Mawaziri na Makatibu Wakuu, kuhakikisha Taasisi zote za Umma, zinatumia mfumo wa wa kielekroniki wa Manunuzi ya Umma - NeST katika manunuzi yote ya Serikali ili kuongeza tija na ufanisi.



Mhe.Dkt.Biteko ametoa maagizo kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. Samia, Suluhu wakati akifungua Jukwa la 16 la Ununuzi wa Umma, kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimatifa Arusha, Septemba 09,2024.



“Ninawaelekeza pia Mawaziri na Makatibu Wakuu wote kuhakikisha kuwa Taasisi zilizochi chini ya Wizara zenu, kuhakikisha zinautumia mfumo wa NeST,  ninashangazwa kusikia, pamoja na jitihada za Serikali kuwa na mfumo wa NeST, kuna baadhi ya Taasisi za Umma hazitumii mfumo huo katika shughuli za ununuzi"Amesisitiza Dkt.Biteko



Aidha, amemuelekeza Waziri wa Fedha kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine, kuhakikisha wote waliopewa jukumu la kuongoza Taasisi za Umma kutumia mfumo wa NeST, ili kujihakikishia usahihi na udhibiti wa fedha za Serikali.



Ameongeza kuwa, kwa Tanzania mfumo huo, umeleta manufaa makubwa kwa kupunguza gharama za matumizi ya karatasi, kuongezeka kwa kasi ya ununuzi,kupungua kwa makosa katika ununuzi na kuboresha utoaji huduma kwa wazabuni na wananchi.



“Nimefurahi kusikia  mfumo huu pia umeongeza uwazi, uwajibikaji na kuleta thamani ya fedha katika ununuzi ni wazi kuwa mfumo huu utaleta faida nyingine nyingi ikiwemo kuimarisha utawala bora,kuongeza wigo wa ununuzi na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa".Ameongeza.



Aidha alisema Serikali imeendelea kudhibiti matumizi ya fedha zinazopelekwa kwenye kila fungu kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mifumo ya kielektroniki ili kuleta tija na ufanisi unaostahili katika utekelezaji wa Bajeti ya fungu husika.



Hata hivyo amekiri kuwa, Tanzania imefanya mageuzi makubwa ya kisheria katika ununuzi wa umma ambayo yalianza Mwaka 2001 kwa kutungwa kwa sheria ya kwanza ya Ununuzi wa Umma, baada ya changamoto kadhaa, zilizosababisha mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2004, na kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa