TAARIFA KWA UMMA/VYOMBO VYA HABARI
IBAADA MAALUM YA KUMBUKIZI YA MIAKA 40 YA KIFO CHA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, inapenda kuutaarifu Umma kuwa, kutakuwa na Ibada Maalum ya Kumbukizi ya miaka 40 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya kwanza, Hayati Edward Moringe Sokoine, itakayofaanyika kesho tarehe 12 Aprili, 2024 nyumbani kwake, kijiji cha Enguik kata ya Monduli juu, Wilaya ya Monduli.
Viongozi Wakuu wa Chama na Serikali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan watashiriki Ibada hiyo Maalum ya Hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki Dunia tarehe 12. 04.1984.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, anawakaribisha wageni na wananchi wote wa Mkoa wa Arusha kushiriki Ibada hiyo Maalum, kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa maisha ya Hayati Edward Moringe Sokoine aliyoishi duniani na kipindi chote alichowatumikia watanzania kwa nafasi mbalimbali ikiwemo nafasi ya Waziri Mkuu.
Aidha, wageni waalikwa na wananchi wote wanasisitizwa kufika eneo la Ibada mapema, kuanzia saa 12: 00 asubuhi mpaka saa 02:30 asubuhi, ili kuruhusu shughuli za viongozi Wakuu wa Nchi na Kanisa kuwasili na kuanza Ibada kwa wakati.
Kudhuria kwenu ni muhimu ili kudumisha umoja na mshikamano wetu kwa maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
OFISI YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa