Na Prisca Libaga
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu was Rais Mary Maganga amesema Serikali ya Tanzania imejipanga vyema katika sera za utunzaji wa Mazingira kuendana na mabadiliko ya tabia ya Nchi katika Maeneo Nyeti ya kilimo na Uchumi Wa Buluu pamoja na Maeneo yanayoathirika Sana ya Mazingira Asili ikiwemo Matumizi ya Nishati Safi.
Maganga ameyasema hayo Jijini Arusha Akifungua kikao cha Kitaifa cha Wadau wa Maandilizi ya Mkutano wa Nchi Mwanachama wa Mkataba wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi ( COP28) utakaofanyika Dubai , Umoja wa Falme za Kiarabu, kuanzia November 30 hadi December 12 2023.
Awali akiongea katika kikao hicho Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Mazingira Dkt. Omar Shajak amesema Madhumuni ya Kikao hicho ni kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa 28 wa Mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika nchi za Falme za kiarabu Dubai.Ambapo masuala mbalimbali yatazungumziwa ikiwa ni pamoja na Uchumi wa Buluu.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi ofisi ya Makamu wa Rais , Mazingira Dkt. Paul Deogratius ametaja dhamira Kuu ya wajumbe hao kukutana hapa Jijini Arusha ni kamati tendaji kujadili kwa pamoja yaliyojiri kwenye kikao cha 27 ( COP27) mafanikio, changamoto na mwelekeo kuelekea COP28.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa