Tanzania imeanza utekelezaji wa Mpango wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto ambapo unalenga kuboresha huduma mbalimbali za Afya, kama vile; Ujenzi wa vituo vya Afya, kuajiri watoa huduma za afya kwa Mikataba katika kipindi chote cha utekelezwaji wa mpango huu na kuendelea kuboresha Huduma ya M – mama.
Mpango huo unatekezwa kwa kipindi cha Miaka Mitano, unatekezwa kwa pamoja kati Wizara ya Afya Tanzania Bara, Ofisi ya Rais –TAMISEMI na Wizara ya Afya - Zanzibar na kuratibiwz na Wizara ya Fedha Tanzania bara na Wizara ya Fedha, Tanzania Zanzibar.
Akiwasilisha mpango huu Katika Mkutano wa Nane wa Tathimini ya Mkataba wa lishe na Kutambulisha Mpango wa Taifa wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto (TMCHIP) uliofanyika katika ukumbi wa Jiji Mtumba Jijini Dodoma Dr. Athumani Pembe ambaye ni Mratibu wa Mpango huu amesema mpango huo umelenga Kuboresha huduma za Afya ya uzazi za dharura na upasuaji kwa akina Mama Wajawazito, kuboresha huduma za dharura kwa Watoto wachanga na Watoto wanaougua na Kuimarisha utoaji wa huduma za afya ya uzazi kwa vijana balehe.
Melengo mengine ni Kuimarisha afua za lishe kwenye Mikoa na Halmashauri, Kuimarisha mfumo wa rufaa na magonjwa ya dharura katika Ngazi ya Afya ya Msingi na Hospitali za Rufaa za Mikoa pamoja na Kuimarisha mifumo ya TEHAMA kwa ajili ya ukusanyaji na uchakataji wa takwimu mbalimbali za afya.
Mkutano huo ambapo Mgeni wake Rasmi ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa umehudhuriwa na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga wa Kuu wa Mikoa na wa Wa halmashauri na Maafisa lishe wa Mikoa.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa