Na Elinipa Lupembe.
Mjasiriamali wa Kikundi cha Naisura cha Olasiti jijini Arusha, Bi. Tatu Ramadhani Hongwa, akimpa zawadi ya bidhaa za sabuni zinazotengenezwa na kikundi hicho, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB), muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Maadhimisho ya 3 ya Wiki ya
Huduma za Kifedha Kitaifa yanaendelea mkoani Arusha, kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha, leo tarehe 22.11.2023.
Kikundi cha Naisura ni miongoni mwa vikundi vya wajasiriamali vinavyoundwa na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, unaoratibiwa na Serikali, kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ( TASAF).
Hata hivyo Waziri Mkuu amewaponheza wanufaika hao wa TASAF na kuwataka, kuendelea kuimarisha vikundi vya kuweka na kukopa, kupitia ruzuku ya fedha wanazopokea ili kuaota mitaji ya kuanzisha biashara ndogondogo zitakazowawezesha kukuza pato la Kaya.
"Nimefurahisgwa sana na vikundi vya wajasirira mali, vinavyoundwa na wanufaika wa TASAF, kwa kutumia fedha za ruzuku wanazopokea, wajasiriamali hawa, wanatekeleza malengo ya serikali ya mpango wa TASAF wa kuondoa uamsikini uliokidpthiri kwenye kaya" Amebainisha Mhe. Majaliwa
Awali, Maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha kitaifa 2023, yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu na yanafanyika kwa siku 5, kuanzia tarehe 20 - 26 Novemba, 2023 yenye kauli mbiu Elimu ya Huduma za Fedha ni Msingi
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa