Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amewaonya vikali wakuu wa idara mbalimbali za serikali ambao hawafanyi kazi zao kwa weledi hadi kusubilia ukaguzi wa viongozi wakuu.
Gambo amesema hayo wakati akiutimisha ziara yake ya siku ya kwanza ya ukaguzi wa ujenzi wa viwanda vipya jijini Arusha katika kiwanda cha MONABAN TRADING COMPANY LTD cha utengenezaji wa mifuko kilichopo katika kata ya moshono jijini Arusha.
Gambo ameeleza kwamba kumekuwa na uzembe mkubwa wa watendaji wa serikali hasa wakuu wa vitengo kutowafuata wawekezaji kujua changamoto zao hadi pale viongozi watakapo fanya ziara katika maeneo mbalimbali kwaajili ya ukaguzi wa maendeleo na watumishi hao kutokuwa na majibu ya kutosheleza kutokana na kujifungia maofisini na sio kufanya kazi za wananchi.
Aidha pia Gambo amemuagiza Katibu Tawala wa mkoa Richard Kwitega kuwafuatilia kwa ukaribu watendaji hao ili kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani hivi sasa ni zama za utendaji kazi na sio zama za kulala na kuwataka kama hawawezi kwenda na kasi ya Dk Magufuli waache kazi mara moja na kuwapisha watu wenyeuwezo.
"Nikutake katibu mkuu wa mkoa kuwafatilia kwa karibu sana watendaji wazembe wanao fanya kwa mazoea waache mara moja kwani hawamu ya tano ni ya utendaji kazi na inamalengo ya kufikia uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda sitaki mzaa katika kazi na nitaakikisha ninakaa na taasisi zote za serikali kama Tanesco, TRA , TANROAD,TARURA pamoja na AUWASA ili kuahikisha changamoto zite zinazo wakabili tunazimaliza." Alisema Gambo.
Aidha Mrisho Gambo aliwahakikishia wawekezaji wote wa jiji la Arusha kuwa serikali ya awamu ya tano ipo tayari kuwapokea na kuwajali kani dhumuni la serikali ni Tanzania ya viwanda na kuwataka waweke kipaumbele kuwaajili watanzania na kuwapongeza wakezaji hao kwa ujasili na ukomavu wa kuweza ndani ya wa muwekezaji wa kiwanda cha MONABANI TRADING COMPANY LTD, Ndg Philemon Mollel ( MONABANI ), ameweza kuiomba serikali kupunguza kodi za tozo kwa kuagiza malighafi nje ya nchi kwa ajili ya utengenezaji mifuko hiyo hapo kiwandani ili kuweza kumudu gharama za uwekezaji.
"Nikuombe mkuu wa mkoa kutufikishie changamoto zetu za ukubwa wa kodi zinatufanya tushindwe kuwekeza na kuendesha viwanda ndani ya nchi tuiombe serikali utufikilie upya katika tozo ili tuweze kuendana na kaulimbiu ya serikali ya viwanda" Alisema Mollel.
Awali akisoma lisara ya ujenzi wa kiwanda mkurugenzi wa fedha wa kampuni hiyo Nathan Mollel ameeleza kuwa hadi kukamilika kwa kiwanda hicho kitaghalimu jumla shilingi Bilioni 9.6 na na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya mifuko milioni moja kwa mwaka huku kikiwa kimetoa ajira kwa watanzania wasio pungua 150.
Ziara hiyo ya mkuu wa mkoa iliyoa anza leo ya kutembele viwanda nane vipya vinavyo jengwa katika jiji la Arusha na inategemewa kumalizika tarehe March 23 mwaka huu ambapo anatembelea viwanda vya Athere to ideal making Ltd, The Old Moshi Distillery Ltd pamoja na Monaban Trading and Compay Ltd,Tanzania Geomolohical Cetre, International Dairy Product,Bhuni Mbuni Co.Ltd, Swed Tan Ltd pamoja na Sterling Surfactants
Ziara hiyo ya ukaguzi wa viwanda imeanza baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ya kuwataka wakuu wa mikoa yote kuhakikisha kila mkoa unakuwa na viwanda 100 mpaka ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa