Walimu mkoa wa Arusha wamekiri kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, imefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu, tofauti ni huko nyuma, jambo ambalo licha ya kupandisha taaluma na kuongeza idadi ya wanafunzi, limeamsha ari ya walimu na wanafunzi katika tendo la kufundisha na kujifunza.
Haya yamewekwa wazi na walimu wa mkoa huo, wakati wa Kongamano la Wadau wa Elimu kuelekea juma la elimu Mkoa wa Arusha, lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Septemba 17,2025.
Wamethibitisha kuwa, katika awamu ya sita, zimejengwa shule mpya za msingi 14 na sekondari 27, uwepo wa vifaa vya kisasa vya kujifunzia na kufundisha, ujenzi wa nyumba za walimu, upandishaji wa vyeo kwa walimu pamoja na fedha za uendeshaeji elimu bila malipo zilizopelekea ongezeko la idadi ya wanafunzi shuleni.
Mwenyekiti wa Umoja wa shule za Msingi TAPSHA mkao wa Arusha, Mwl. Amani Palangyo amesema kuwa, uwepo wa miundombinu bora na ya kisasa shuleni unawapa moyo walimu kufundisha na kujenga uhusiano baina ya mwalimu na wanafunzi unaorahisisha tendo la kufundisha na kujifunza.
"Mimi kama mwalimu ninayefundisha darasani pamoja na walimu wenzangu tunayo makubwa ya kushuhudia yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita,kwa sasa tunafundisha kwenye madarasa mazuri, madarasa makini yenye vifaa vya kisasa vya kielekroniki vya kufundishia, walimu wanaishi shuleni kwenye nyumba nzuri, kiukweli hatujachwa nyuma".Amesisitiza Mwl.Pallangyo
Naya Mwenyekiti wa Umoja wa alimu wa Shule za Sekondari - TAHOSA Mkoa wa Arusha Mwl. Omari Nyigu amesema kuwa, kwa kipindi cha miaka 4, idara ya elimu sekondari imepokea shilingi bilioni 64.1 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule, miundombinu ambayo imeongeza ari ya wanafunzi kujifunza na walimu kufundisha.
Hata hivyo Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Arusha Mwl.Tumsifu Mushi, ameweka wazi kuwa katika kipindi cha miaka 4 ya serikali ya awamu ya sita, sekta ya limu imepkkea jumlanya shilingi bilioni 171.9 kwa ajli ya shughuli za elimu na shilingi bilioni 107 za ujenzi na ukarabati wa miundombinu.
#kaziinaendelea
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa