Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ameitaka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kufanya uchunguzi wa kina wa sababu inayosababisha wafanyabiashara kutokulipa kodi.
Aliyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi wa kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru mkoani Arusha baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Arumeru.
Magufuli amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara wanawatumia wafanyabiashara wadogo (wamachinga) kuwauzia bidhaa zao ingali wao wanafunga maduka yao kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.
Nchi inaendeshwa kwa kodi za wananchi hata mradi huu wa maji niwa mkopo wa riba ya bei nafuu kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na wananchi ndio mtalipa deni hili kwa kulipa kodi.
Amewahasa wananchi kulipa kodi kwa ustawi wa maendeleo ya nchi kwani miradi mingi ya maendeleo inategemea kodi za wananchi,hivyo niwatake wamachinga kutokukubali kutumiwa na wafanyabiashara wakubwa ili wakwepe kodi.
Pia,ameiagiza TRA kuangalia tena viwango vyake vya tozo za kodi kwani huwenda viwango ni vikubwa sana vinavyowafanya wafanyabiashara wengi kukwepa kulipa kodi kwani ni bora kuwa na viwango vidogo ili wengi walipe kuliko viwango vikubwa vinavyowashinda kulipa.
Amesema elimu pia inaitajika kwa wananchi juu ya umuhimu wa ulipaji kodi kwa wananchi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Magufuli aliweka jiwe la msingi katika mradi wa maji utakaogharimu kiasi cha bilioni 520 mpaka kukamilika na utakuwana na uwezo wakuzalisha lita million 208 kwa siku.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa