• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WA SAMUNGE WILAYANI NGORONGORO WAPATIWA CHUO CHA UFUNDI

Posted on: May 18th, 2023

Makamu wa Rais, Dkt.Philip Mpango  ameagiza Wizara ya Fedha kutoa kiasi cha shilingi milioni 290 kwa ajili ya kumalizia ujenzi  wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kilichopo Samunge Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha.

Aidha ametoa rai kwa vijana wa kike na wakiume kwenda Veta kusomea fani mbalimbali ikiwemo Ufundi wa kushona nguo badala ya kuwaachia mafundi wanawake pekee kwa kuwa ni fani ambayo vijana wanaweza kujiajiri.

Dkt.Mpango ametoa agizo hilo jana katika Kata ya Samunge  wilayani Ngorongoro wakati akifungua rasmi chuo cha VETA kilichojengwa wilayani humo ambapo awali ujenzi wake ulianzishwa  na vijana wa kabila la  wasonjo wa rika la erumeshari.

"Wizara ya fedha hakikisheni mnaleta mara Moja kiasi cha fedha shilingi milioni 290 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa chuo hiki  ujenzi wake ulianzishwa na rika la Erumeshari kisha kuungwa mkono na serikali ili wanafunzi ambao wameshaanza masomo ya fani mbalimbali katika chuo hiki wasipatwe na changamoto zozote".

Katika hatua nyingine  Dkt. Mpango aliwaagiza Wakala wa Barabara Mkoa wa Arusha, (TANROADS) kutengeneza barabara inayokwenda chuoni hapo kutoka barabara kuu ya lami ya Waso- Sale  ili iweke mazingira mazuri ya chuo.

"Chuo hiki ni kizuri kinavutia na wananchi hawa wa jamii ya Kisonjo wameonyesha nia ya watoto wao kupata elimu ya ufundi stadi hivyo nitumie fursa hii kumwagiza meneja wa RUWASA Mkoa wa Arusha kuhakikisha maji ya uhakika yanapatikana hapa chuoni ili wanafunzi wasipatwa changamoto ya maji".

Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Anthony Kasore alisema  mwaka 2023 serikali ilitoa kiasi cha sh.Milioni 272 Kwa lengo la kumalizia kazi zote za ujenzi wa majengo ambayo hayajakamilika.

Alisema chuo hicho kimefanikiwa kudahiki wanafunzi 147 ambapo wasichana ni 68 na wavulana 79 katika fani ya umeme,ubunifu wa mavazi,ushonaji na Teknolojia ya nguo na uashi.

Lakini pia miundombinu ya barabara  inahitajika kwani barabara hiyo nyakati za mvua haipitiki na kupeleka ongezeko la gharama za usafiri sanjari na uhitaji wa Nyumba za watumishi pamoja na ukosefu wa uzio unaozunguuka chuo hicho unaopelekea uvamizi wa wanyana na wananchi.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella  amesema eneo la Samunge ni maarufu sana kwani watu walikuwa wakienda kupata kikombe cha babu wa Loliondo.

Alisema Samunge ni eneo la kimaendeleo kutokana na mfumo wao wa kimila kwa wanarikal la erumeshari  jamii ya Wasonjo kutoa mchango mkubwa wa kimaendelo na wanalima na kufuga pia.

"Nawapongeza watu wa eneo hili kwa kusimamia dhana nzima ya maendeleo,endeleeni kuleta maendeleo".

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa