Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro wamehimizwa kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi Novemba, 2024 huku wakichukua tahadhari kubwa na viongozi wanawarubuni kwa zawadi ili wawaingize madarakani.
Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava wakati akizindua Klabu ya Wapinga Rushwa shule ya Msingi Monic kata ya Engariselo wilaya ya Ngorongoro leo Julai, 25, 2024.
Kupitia igizo walilolifanya wanakalabu hiyo, namna wananchi walivyorubuniwa na kiongozi wao kwa kuepewa rushwa na kumchagua, baada ya uchaguzi kiongozi huyo hakutokea mpaka uchaguzi mwingine ulivyokaribia.
Amewakumbusha wananchi kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa ni uchaguzi wa kisheriq ambapo wananchi wanalojukumu kubwa la kuchagua kiongozi mwenye sera na sira za kuwaongoza na mwenye uzalendo wa nchi yake nq kuwatumikia na sio anayetoa rushwa.
Ameongeza kuwa, wananchi wanatakiwa kuzingatia uchaguzi huru na wa haki, na kutokukubali kudanganywa na zawadi za aina yoyote ikiwemo fedha na kuwataka kumuogopa na kumkataa kiongozi wa aina hiyo.
"Ndugu zangu tusikubali kudanganywa na Rushwa, tuchague viongozi kwa haki kwa kuzingatia Sera bora za viongozi watakaogombea ili kupata viongozi watakaotuongoza na kutupeleka kwenye maendeleo katila maeneo yetu".Amesema
Aidha wamehimiza kuikataa na kuichukia rushwa kwa kuwa rushwa ni adui wa haki, wapo watu wengi wameumizwa kutokana na vitendo vya rushwa, kwa kufanya hivyo hivyo tutakuwa na Tanzania salama ya watenda haki.
Hata hivyo amewapongeza wanafunzi wa klabu ya wapinga Rushwa na kuwasisitiza walimu kuongeza nguvu ya kuwafundisha watoto hao masuala ya haki na Rushwa , ili kuwa na kizazi cha watenda haki na wenye uzalendo katika kulitumikia Taifa la Tanzania.
Akisoma taarifa ya Klabu , Mwenyekiti wa Klabu hiyo Jasmini Mjuni, amesema kuwa klabu yao ina wanachama 40, ambao licha ya kufundishwa masuala ya mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa wamekuwa wakiwafundisha wanafunzi wenzao na wazazi wao nyumbani
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchagu
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa