Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuandikisha Wapiga Kura wapya 224,499 sawa na ongezeko la 18% ya wapiga kura 1,225,584 walio kwenye daftrai la Wapiga Kura mkoa wa Arusha.
Idadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Kailima (INEC) Kailima Ramadhani
wakati wa Mkutano wa wadau wa Uchaguzi na Tume ya uchaguzi, ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoa wa Arusha, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Novemba 29,2024.
Amesema kuwa baada ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kufanyika kwa siku saba mkoani Arusha kuanzia Novemba 11 -17, 2024, mkoa wa Arusha utakuwa na jumla ya Wapiga Kura 1,480,083.
Hata hivyo ameongeza kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa kuwa wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa Uboreshaji wa Daftari uliofanyika mwaka 2019/2020
Amefafanua kuwa, Tume imeridhia mabadiliko ya idadi ya vituo vya kujiandikishia Wapiga Kura kutoka vituo 40,126 na kufikia Vituo 40,170 kwa kurejesha vituo 44 vya kata 11 za Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro.
"Kwa mkoa wa Arusha kuna vituo 1,454 vitakavyotumika kwenye zoezi la Uboreshaji wa Daftari la wapiga mwaka huu wa 2024 ikiwa ni onhezeko la vituo 88 katika vituo 1,368 vilivyotumika mwaka 2019/2020".Amefafanua Kailima.
Aidha ameeleza kuwa, zoezi la uboreshaji Daftari la Kudumu, utahusisha wapiaga Kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapoa tarehe ya Uchagui Mkuu 2025, kuboresha taarifa za wapiga Kura waliohama, waweze kuhamisha taarifa zao.
Ameongeza kuwa, zoezi hilo litatoa fursa kwa wapiga Kura wanaotaka kurekebisha taarifa zao ikiwemo majina na taarifa nyingine, kutoa kadi mpya kwa Wapiga Kura waliopoteza kadi zao ama kuharibika, kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo pamoja na kuukana uraia wa Tanzania.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa