Halmashauri ya Wilaya ya karatu imewadhamini wateja wake kwa kuwaandalia cake pamoja na Kupata chai asubuhi ofisini ikiwa ni kuazimisha wiki hii maalumu ya Huduma kwa Mteja.
Akizungumza baada ya hafla hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Ndg. @hokororojuma amesema watumishi wa halmashauri licha ya wiki hii wataendela kutoa huduma bora kwa wananchi wa karatu bila kujali hali ya mtu.
Aidha amewataka watumishi wa Halmashauri kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa wakati kwa wananchi ili kuendelea kutekeleza adhma ya serikali ya awamu ya sita na kuwafikia wananchi kwa wakati.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa