“Nendeni mkasimamie fedha zote za miradi ya maendeleo zinazoletwa na serikali katika maeneo yenu”.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Kimanta alipofanya kikao kazi na watumishi wa halmashauri ya Arusha katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Amesema, serikali inaleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo watendaji wote wa serikali wakahakikishe zinatumika kama ilivyopangiwa bila kuwa na upotevu wowote.
Pia, amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kufanya kazi kwa amani, upendo na kwa kushirikiana kwani kila mmoja ana mchango wa kumuinua mwenzake katika utumishi wa umma.
Nae, Mkuruenzi wa halmashauri hiyo bwana Saad Mtambule, amesema halmashauri yake inaendelea kusimamia kwa umakini miradi yote ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
Bwana Mtambule amesema pia hata stahiki za watumishi anaendelea kuzisimamia kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya serikali kwa kuhakikisha haki inatendeka kwa watumishi wote.
Akitoa neno la shukrani Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Arusha Bi.Angela Avaa amesema, wamefurai sana kupata mawaidha mazuri kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na wapo tayari kuyafanyia kazi yote kwa ujenzi bora wa halmashauri hiyo.
Mkuu wa Mkoa amekutana na kuzungumza na watumishi hao kwa lengo la kutoa maelekezo ya namna ya kutekeleza majukumu yao katika utumishi wao wa Umma.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa