WALIOFANYA UHALIFU WA KUPORA KWA PIKIPIKI WAKAMATWA ARUSHA.
Na.Abel Paul, Jeshi la Polisi- Arusha.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linamshikiria mtuhumiwa aliyeonekana katika video ambayo ilisamba katika mitaandao ya Kijamii na kupora vitu kwa mwananchi mmoja huko maneo ya Burka kisongo Jijini Arusha.
Akitoa taarifa hiyo leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema Jeshi hilo lilipata taarifa kupitia mitandao ya Kijamii ambapo ili waonyesha vijana wawili wakiwa na pikipiki na kumpora mwanamke mmoja huko maeneo ya Burka kisongo jijini Arusha.
Aidha amesema mara baada ya kupata taarifa hiyo mara moja walianza uchunguzi wa kina na kuwatambua wahusika wa tukio hilo ambapo Machi 28,2024 mtuhumiwa Jamal Idd Ramadhan (22) mkazi wa Ngusero alikamatwa.
Jeshi hilo limebainisha kuwa katika Uchunguzi wa Tukio hilo ulipofanyika ulibaini watuhumiwa hao walimpiga na kitu chenye ncha kali mwanamke huyo ambae jina lake halikuweza kufahamika ili kumuhadaa na kumtisha waweze kumpora vitu alivyokuwa navyo mwananchi huyo.
Aliendelea kuviambia vyombo vya habari kuwa Jitihada za kuwatafuta wengine zinaendelea ili kuutambua mtandao wao wa uhalifu.
SACP Masejo amesema Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linaendelea kuwashukuru wananchi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu Pamoja na waandishi wahabari kwa kufichua uhalifu katika Mkoa huo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa